TwitterPinterest Facebook Emailyoutube

Wednesday, 6 April 2016

0

NIKKI MBISHI ATANGAZA KUSITISHA KUWEKA NYIMBO ZAKE MKITO.COM

Msanii nguli wa hip hop Nikki Mbishi ametangazakupitia akaunti yake ya instagramkwamba atasitisha kuitumia tovuti maarufu kwa mauzo ya nyimbo za wasanii ya Mkito.com kutokana na usumbufu wa upatikanaji wa kazi zake katika site hiyo au sivyo warudishe muonekano wao uwe kamazamani.
#SAMAHANINI_MASHABIKI_WANGU Kumekuwa na malalamiko ya watu kushindwa kudownload kazi za wasanii especially mimi na complications za hapa na pale ambazo ni kero kwa watumiaji wa site ya @mkitodotcom licha ya nguvu na muda ninaowekeza kupromote.  #MAAMUZI_YANGU Mimi Nicas J. Machuche(Nikki Mbishi), kufuatia kutoridhishwa na utendaji wa site ya MKITO.COM,nimeamua kusitisha kutoa kazi zangu kwenye site hiyo.  Tangu yafanyike mabadiliko ya muonekano wa site hiyo kumekuwa na kero nyingi kutoka kwa watumiaji wa kawaida yaani wasanii na mashabiki.  Pia nimejikuta nikitumia nguvu na muda mwingi kupromote biashara isiyo na faida kwangu kwa kipindi hiki kifupi cha mabadiliko ya site, hivyo kwa kufuata taratibu husika nikiwa kama mmliki halali wa kazi zangu na nina mamlaka nazo, nimeamua kufunga account yangu ya mkito i.e nasitisha kazi zangu kupatikana site hiyo.  Mimi kama mlengwa nisiposikilizwa ninapolalamika atasikilizwa nani?Mlianza vizuri ila kwa sasa mmeelemewa na wingi wa watumiaji site na mmeshindwa kuboresha huduma zaidi ya kuzorotesha ufanisi.  Maoni na maombi yangu binafsi ni aidha mrudishe muonekano wa zamani ama sitoweza kuendelea biashara nanyi.  Asanteni.
A photo posted by ICONICAS (@nikkimbishi) on

0 comments: